Sample Sidebar Module

This is a sample module published to the sidebar_top position, using the -sidebar module class suffix. There is also a sidebar_bottom position below the menu.

Sample Sidebar Module

This is a sample module published to the sidebar_bottom position, using the -sidebar module class suffix. There is also a sidebar_top position below the search.
Idara ya Mawasiliano

Idara ya Mawasiliano ni idara inayoandaa , kuboresha na kusimamia sera ya TEHAMA na kutoa ushauri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yote yanayohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano Zanzibar.Idara hii ina jukumu la kusimamia huduma za mawasiliano na masuala ya Taasisi za Mawasiliano za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zilizopo Zanzibar. Idara pia, ina jukumu la kuratibu na kusimamia uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano. Idara inaendelea kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa Zanzibar, kuendelea kuandaa Sheria na Kanuni za TEHAMA na Mpango Mkakati wa TEHAMA. Idara pia ina jukumu la kusimamia mkonga wa mawasiliano kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel kwa upande wa matumizi ya Serikali na Taasisi binafsi.

TAASISI ZA MUUNGANO SEKTA YA MAWASILIANO

Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imeendelea kushirikiana na Taasisi za Muungano zilizopo hapa Zanzibar katika utoaji wa huduma na usimamizi wa Sekta ya Usafiri na Mawasiliano. Miongoni mwa Taasisi za Muungano tunazoshirikiana nazo ni:- Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Tanzania (TMA), Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA), Shirika la Posta la Tanzania (TPC) na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA). Mashirikiano naTaasisi yamechangia sana kukuza Sekta ya Usafiri na Mawasiliano hapa Zanzibar.

MAFANIKIO YA IDARA YA MAWASILIANO..

Idara ya Mawasiliano inasimamia na kuimarisha huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano hapa Zanzibar.Idara imefanya matengenezo ya mkonga wa taifa maeneo yalioharibika katika barabara ya Tunguu – Istiqama, Kiwengwa, Paje na Nungwi Unguja. Kwa upande wa Pemba hatua za matengenezo zinaendelea katika maeneo mbali mbali kama vile Machomane, Wete, Kwale, Kizimbani, Kiungoni na Kifumbikai zimekamilika.Aidha, uwekaji “Alarm System” kwenye vituo vyote 12 vya mkonga vilivyopo Zanzibar umefanyika ili kuvilinda na kuviwezesha kutoa taarifa Makao Makuu pale maharibiko ya aina yoyote yatakapotokezea.

kuhusu uunganishwaji wa Mkonga kwenye taasisi za Serikali, hadi kufikia Machi 2015, taasisi 84 tayari zimeunganishwa na mkonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel, ikiwa taasisi 50 zinatumia huduma hiyo na taasisi 34 zipo katika hatua za mwisho za kuwekewa vifaa husika ili nazo ziweze kutumia huduma hii.

Wizarakwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ya SMT imeweka mitambo ya mawasiliano picha (Video Conference) katika sehemu 5 tofauti Unguja na Pemba na mitambo hiyo inafanya kazi. Aidha, Wizara kwa kushirikia na Kampuni ya ZTE ya China imefunga computer 50 kwa ajili ya Kituo Jamii cha TEHAMA katika skuli ya Kiembe Samaki na kuunganishwa na mkonga wa Taifa.

MALENGO YA IDARA

  1. Kujenga, kusimamia na kuendesha vituo kadhaa vya TEHAMA JAMII (Telecenters)katika kila wilaya ya Unguja na Pemba vitavyowezesha jamii kupata uwelewa na kujifunza kuhusu matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano.Hii pia itahusisha upatikanaji wa huduma za TEHAMA kwa urahisi na kwa bei nafuu.
  2. Kuandaa sheria juu ya usimamizi , udhibiti na matumizi salama ya TEHAMA pamoja na sheria ya usimamizi wa miundombinu ya mawasiliano kama vile mkonga na minara.
  3. Kuweka na kusimamia  mitambo ya mawasiliano picha (video conference) katika taasisi mbali mbali za serikali. Hii ni pamoja na kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitambo hiyo kwa wadau watakaotumia.
  4. Kuuboresha Mkonga wa mawasiliano wa Zanzibar, kwa kuuwekea vifaa vya kisasa pamoja na kuziunganisha taasisi nyengine mbali mbali za serikali na binafsi kwa kutumia mkonga huo.
  5. Kuweka mpango mkakati wa kutekeleza na kusimamia sera ya mawasiliano ya Zanzibar (Zanzibar ICT policy)
  6. Kusimamia Ujenzi wa minara na wa miundombinu mengine ya mawasiliano.
  7. Kusimamia na kuratibu uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano ya anuwani za makaazi. (postcode) katika shehia zote za Unguja na Pemba.
  8. Kuratibu na kusaidia Uunganishwaji wa watoa huduma wote wa internet waliopo Zanzibar baina yao ili kuhakikisha mawasiliano yote ya Zanzibar yanabakia Zanzibar. Hii itapunguza gharama za internet na inaongeza kasi ya  huduma hiyo kwani itaondoa mfumo uliopo sasa wa ujumbe wowote wa internet kwenda kwanza marekani au ulaya kabla ya kumfikia mlengwa

 

Kurasa za Karibu