Sample Sidebar Module

This is a sample module published to the sidebar_top position, using the -sidebar module class suffix. There is also a sidebar_bottom position below the menu.

Sample Sidebar Module

This is a sample module published to the sidebar_bottom position, using the -sidebar module class suffix. There is also a sidebar_top position below the search.
Kitengo cha mkonga

MKONGA WA MAWASILIANO WA TAIFA

Idara ya Mawasiliano iliyopo chini ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ndiyo iliyokabidhiwa jukumu la kusimamia mkonga wa mawasiliano wa Taifa na kuhakikisha Serikali inafaidika kutokana mradi huo.

Kutokana na mkataba wa makubaliano ya mashirikiano yaliyosainiwa tarehe 15 mwezi wa Febuari  2013  baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Zantel kwa ajili ya uwekaji na uunganishaji wa mkonga wa mawasiliano. Kiambatanisho namba moja kiliitaka Zantel kuzifikishia na kuziunganisha mkonga Taasisi 84 za Serikali.

Uunganishaji wa mkonga kwa Taasisi za Serikali:

Jumla ya Taasisi 84 Unguja na Pemba zimefikishiwa mkonga wa mawasiliano kwa hatua ya Optical Distribution Frame (ODF) kati ya hizo  hamsini na nne (54) zimeshafungiwa  vifaa vya mkonga wa mawasiliano kwa hatua ya matumizi kwa upande wa Unguja na tayari zinaonana na makao makuu ya Serikali mtandao Mazizini Zanzibar ikijumuisha na Wizara ya Ardhi Pemba. Aidha Idara ya Mawasiliano ipo mbioni kuhakikisha zoezi linaendelea kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel pamoja na Idara ya Serikali Mtandao (E-Government) ya kuhakikisha Taasisi zilizobaki kwa upande wa Pemba zinapatiwa vifaa vya kuziunganisha na kuziwezesha kupata huduma zilizokusudiwa.

Kurasa za Karibu