Sample Sidebar Module

This is a sample module published to the sidebar_top position, using the -sidebar module class suffix. There is also a sidebar_bottom position below the menu.

Sample Sidebar Module

This is a sample module published to the sidebar_bottom position, using the -sidebar module class suffix. There is also a sidebar_top position below the search.
Home

KWA ZANZIBAR YENYE MAWASILIANO BORA

Matukio Katika Picha

Ijue Idara ya Mawasiliano

Idara hii ina jukumu la kusimamia huduma za mawasiliano na masuala ya Taasisi za Mawasiliano za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zilizopo Zanzibar. Idara pia, ina jukumu la kuratibu na kusimamia uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano.

Idara inaendelea kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa Zanzibar, kuendelea kuandaa Sheria na Kanuni za TEHAMA na Mpango Mkakati wa TEHAMA.

Idara pia ina jukumu la kusimamia mkonga wa mawasiliano kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel kwa upande wa matumizi ya Serikali na Taasisi binafsi.

MAKAMPUNI YA SIMU

ZANTEL, TTCL, VODACOM,TIGO,AIRTEL AND VIETTEL

TAASISI ZA MUUNGANO SEKTA YA MAWASILIANO

Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imeendelea kuratibu masuala ya mawasiliano kwa Soma Zaidi

    

UJUMBE KUTOKA MKURUGENZI MAWASILIANO

Maendeleo ya sayansi na teknolojia ya habari  yameleta mageuzi makubwa katika maisha ya mwanadamu pamoja na maendeleo yake kwa ujumla , hivi leo tunashuhudia kuona matumizi ya Tehama yanavotumika ili kukuza uchumi katika mataifa mbali mbali duniani .

Matumizi ya Tehama yanapunguza gharama katika uzalishaji ,  utoaji huduma na uendeshaji  katika sekta mbali mbali za kiserikali pamoja na za kijamii, hivyo basi hatuna budi kujifunza na kutumia fursa hiyo ili kujiletea maendeleo pamoja na kuondoa umaskini.

Halikadhalika TEHAMA hivi leo inatumika katika  sekta za elimu, sekta za afya ili kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi za makusudi imejenga miundombinu ya mawasiliano ya mkonga ili kuboresha huduma za mawasiliano hapa Zanzibar. Hivyo basi miundombinu hiyo ni muhimu kulindwa ili isije ikahujumiwa na kusababisha kuzorota kwa huduma za mawasiliano nchini kwani miundombinu hiyo huchangia shughuli za kiuchumi pamoja na zile za kijamii kutoka Zanzibar kwenda duniani kote kwa kupitia mkonga wa kimataifa.

 

Majukumu ya Idara ya Mawasiliano - Zanzibar


 • Mkonga wa Mawasiliano

  Huu ni miundombinu ya mawasiliano iliyatandikwa ardhini kwa lengo la kurahisisha mawasiliano ya kasi na ya gharama nafuu. Huu ni miundombinu ya mawasiliano iliyatandikwa ardhini kwa lengo la kurahisisha mawasiliano ya kasi na ya gharama nafuu.
   

 • Minara ya Mawasiliano

  Idara ya Mawasiliano inajukumu la kusimamia minara ya mawasiliano iliyopo nchini. Kwa sasa kuna minara Zaidi ya 229 inayotoa huduma za mawasiliano nchini. Idara ya Mawasiliano inajukumu la kusimamia minara ya mawasiliano iliyopo nchini. Kwa sasa kuna minara Zaidi ya 229 inayotoa huduma za mawasiliano nchini.
   

 • Anuwani za Makazi - Postikodi

  Idara ya Mawasiliano inaratibu zoezi zima la uwekaji wa anuwani za makazi nchini zinazojulikana kama postikodi. Mfumo huu unarahisisha utambuzi wa mitaa na kuweza kumfikia mlengwa kwa urahisi Zaidi. Idara ya Mawasiliano inaratibu zoezi zima la uwekaji wa anuwani za makazi nchini zinazojulikana kama postikodi. Mfumo huu unarahisisha utambuzi wa mitaa na kuweza kumfikia mlengwa kwa urahisi Zaidi.
   

 • Sera ya TEHAMA

  Sera ya TEHAMA ina lengo la kukuza matumizi ya Teknologia ya kisasa inayohusu habari na mawasiliano nchini. Matumizi ya TEHAMA huleta urahisi wa uendeshaji shughuli mbalimbali pamoja na kukuza uchumi.
   

 • Vituo vya TEHAMA

  Vituo hivi hutoa mafunzo ya TEHAMA kwa jamii kwa lengo la kukuza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi ya teknolojia hiyo. Mafunzo hayo hutolewa bure kwa wanachi katika vituo hivyo